Watumishi TASAF washiriki mkutano ufuatiliaji na tathimini Zanzibar

By Faustine Feliciane , Nipashe
Published at 05:53 PM Sep 19 2024
akamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Hemed Suleiman Abdulla
Picha:Mpigapicha Wetu
akamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Hemed Suleiman Abdulla

BAADHI ya watumishi wa Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF) wameshiriki Kongamano la tatu la Ufuatiliaji na Tathimini unaofanyika Zanzibar na kushirikisha wadau kutoka sekta mbalimbali.

Akizungumza na Nipashe leo, Mtaalamu wa Masuala ya TEHAMA wa Mfuko huo, Peter Lwanda, amesema wanashiriki mkutano huo ili kujifunza na kuongeza ujuzi katika kufanya tathimini na ufuatiliaji.

 "Kitengo kama hiki sisi TASAF tunacho muda mrefu, lakini kwa sababu tunafanya ufuatiliaji na kufanya tathmini kwenye miradi yetu mbalimbali, mkutano huu ni muhimu kwetu kuongeza ujuzi na kuendelea kujifunza ili kuwa na uhakika wa kufanya kazi kwa ufasaha," amesema Lwanda.

 Amesema TASAF wamekuwa wanaendesha miradi mbalimbali Zanzibar na katika mkutano huo, walibainisha mafanikio yaliyofikiwa na walengwa wa mfuko huo visiwani Zanzibar.

1

 "Lakini kwenye suala la tathmini, sisi pia tumekuwa tukijitathmini kwa kutumia wataalamu kutoka nje ya TASAF tukiamini hatuwezi kujitathmini kama tunataka matokeo sahihi, na kikubwa ni kuhakikisha malengo ya mfuko huu yanafikiwa katika kila miradi yake," amesema.

Mkutano huo ulianza Septemba 17 na kushirikisha wadau kutoka sekta mbalimbali. Unafikia tamati leo visiwani humo.