Mgombea Urais kupitia chama cha National League for Democracy 'NLD',Doyo Hassan Doyo,amewaahidi wakazi wa Jiji la Tanga kuwa ,endapo atachaguliwa atawashughulikia watu viongozi wote wa Serikali waliohusika na ubadhirifu wa fedha za ujenzi na ukarabati wa masoko makubwa ya jiji hilo ikiwemo Soko la Mgandini,Makorola na Mlango wa chuma.
Akizungumza leo Oktoba 26 na Wafanyabiashara pamoja na wakazi wa jiji la Tanga. Doyo alisema ,siku za huko nyuma masoko hayo yalishatengewa fedha kwaajili ya ujenzi na ukarabati lakini fedha zote hazijulikani zilikokwenda,
"haya masoko matatu yalishatengewa fedha kwaajili ya ujenzi lakini mengine kwaajili ya kufanyiwa ukarabati lakini mpaka sasa hakuna kinachoendelea kwenye haya masoko,masoko ni machakavu hayafai kuitwa masoko ya Jiji,nikiingia madarakani nitakwenda kuwashughulikia wote waliozitafuna hizi hela mana ni mabilion ya pesa" alisisitiza Doyo
Doyo alisema watakapopata Serikali watajenga Masoko yote matatu yatajengwa kwa Ghorofa tatu ili kulipa hadhi soko hilo jiji la Tanga ambalo linahitaji kuwa la Kisasa ili wafanyabiashara waweze kufanya biashara zao bila kuwepo kwa changamoto zilizopo kwa sasa.
Alisema kwamba katika ujenzi wa soko hilo eneo la chini litakuwa la mbogamboga na katikati watu wa mchele na nafaka huko juu na watu wa nyanya na mambo mengine mtu akija sokoni anamaliza kila kitu.
“Sokoni sio sehemu ya kuuza tu mbogamboga na nyanya bali ni sehemu ya biashara zote mkinichagua kuwa tutakwenda kujenga soko la biashara na nyie muwe watu kwa watu kwa kuwa kwenye soko lenye hadhi na meza za kisasa”alisema
© 2025 IPPMEDIA.COM. ALL RIGHTS RESERVED