Gaza hatarini kukumbwa na njaa

By Mwandishi Wetu , Nipashe
Published at 02:10 PM Jun 26 2024
Ripoti mpya inaonesha hatari kubwa ya njaa inaigubika Gaza.
Picha: Mohammed Salem/REUTERS
Ripoti mpya inaonesha hatari kubwa ya njaa inaigubika Gaza.

SHIRIKA linalofuatilia viwango vya njaa duniani, IPC, limesema Ukanda wa Gaza unaendelea kukumbwa na hatari kubwa ya njaa, kufuatia vita inayoendelea kati ya Israel na Hamas.

IPC imesema katika tathmini yake mpya kuwa zaidi ya watu 495,000, sawa na zaidi ya humusi moja ya wakazi wa Gaza, wanakabiliwa na viwango vikali zaidi vya janga la ukosefu wa chakula.

DW imeripoti kuwa, Shirika hilo limesema kuongezeka kwa mgao wa ugavi wa chakula na huduma za lishe katika eneo la kaskazini mwa Gaza katika kipindi cha Machi na Aprili ulionekana kupunguza ukali wa njaa katika eneo hilo lililotabiriwa kukumbwa na viwago vikubwa vya njaa.