ICC yataka viongozi wa Urusi wakamatwe

By Mwandishi Wetu , Nipashe
Published at 05:16 PM Jun 26 2024
ICC yataka kukamatwa kwa viongozi wa Russia.
Picha: Maktaba
ICC yataka kukamatwa kwa viongozi wa Russia.

MAHAKAMA ya Kimataifa ya Uhalifu (ICC), imetoa hati ya kukamatwa kwa aliyekuwa Waziri wa Ulinzi wa Urusi, Sergei Shoigu na Mkuu wa Majeshi ya Urusi, Jenerali Valery Gerasimov.

Mahakama hiyo imesema kuna ushahidi wa kuridhisha na kuaminika kuwa washukiwa hao wawili wanawajibika kwa mashambulizi ya makombora yaliyofanywa na jeshi la Urusi, dhidi ya miundombinu ya umeme ya Ukraine kati ya Oktoba 2022 na Machi 2023.

Mahakama imeitolea mfano wa mashambulizi ya Urusi, ambayo yalilenga mitambo na vituo vidogo vya Ukraine.

Taarifa ya ICC imesema Shoigu na Gerasimov wanadaiwa kuhusika na kuelekeza mashambulizi kwenye maeneo ya raia na kusababisha madhara makubwa kwa raia, ambayo yote ni uhalifu wa kivita.