Waziri wa Ulinzi Israel atishia kuivuruga Lebanon

By Mwandishi Wetu , Nipashe
Published at 01:45 PM Jun 27 2024
Waziri wa Ulinzi wa Israel Yoav Gallant akizungumza na wanajeshi wake walioko Rafah.
Picha: Ariel Hermoni/Israel Mod/IMAGO
Waziri wa Ulinzi wa Israel Yoav Gallant akizungumza na wanajeshi wake walioko Rafah.

WAZIRI wa Ulinzi nchini Israel, Yoav Gallant amesema taifa lake halitaki vita na Lebanon, huku akionya kuwa hawatasita kuishambulia vibaya kama juhudi za kidiplomasia zitashindwa.

Gallant amewaambia waandishi wa habari akiwa ziarani mjini Washington kwamba hawako tayari kwa vita, ingawa wamejiandaa kwa chochote kinachoweza kutokea.

Amesema Hezbollah wanatambua vizuri kwamba Israel inaweza kuleta uharibifu mkubwa huko Lebanon, kama watapigana vita.

Ameongeza kuwa Jeshi la Israel lina na uwezo wa kuirejesha Lebanon kwenye "zama za mawe", katika vita dhidi ya kundi hilo linaloungwa mkono na Iran.

DW imeripoti kuwa, Maelfu ya watu kaskazini mwa Israel na kusini mwa Lebanon wamekimbia makaazi yao kutokana na mapigano kati ya Hezbollah na jeshi la Israel.