Helikopta yakubeba wagonjwa watakaozidiwa Arusha hii hapa

By Beatrice Shayo , Nipashe
Published at 02:07 PM Jun 24 2024
Helikopta itakayobeba wagongwa watakaozidiwa Arusha hii hapa.

HELIKOPTA kwa ajili ya kubeba wagonjwa ambao watabainika kuzidiwa katika utoaji wa huduma bure za afya kwa wananchi wa jiji la Arusha tayari imeingia katika viwanja vya michezo vya Sheikh Amri Abeid.

Helikopta hiyo iliingia uwanjani hapo majira ya saa 4:45 asubuhi huku ikishangiliwa na wananchi.

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa huduma huyo, Mkuu wa mkoa wa Arusha, Paul Makonda, amesema helikopta hiyo itawachukua wagonjwa waliozidiwa na kuwapeleka moja kwa moja hospitali hata kama ni mkoa wa Dar es Salaam.

"Atajayekuwa amezidiwa atabebwa na Helikopta hata kama unatakiwa kwenda  Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) ama ni Hospitali Taifa ya Muhimbili (MNH) utapelekwa na Helikopta na kupatiwa matibabu," amesema Makonda.

Makonda amesema hata kama kambi hiyo ya matibabu itakuwa imemaliza muda wake wa siku saba waliobainika na matatizo wataendelea kupatiwa matibabu hadi kuimarika kwa afya zao.

"Hapa tumeleta hospitali 37 na kuziweka sehemu moja lengo ni kuwasaidia wananchi kupata matibabu na upande wa dawa zipo za kutosha hakuna atakayeondoka bila dawa," amesema Makonda