Mazuri ya dira 2025 yawe msingi wa dira 2050- Prof. Mkumbo

By Maulid Mmbaga , Nipashe
Published at 02:59 PM Jan 08 2025
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Mipango na Uwekezaji Prof. Kitila Mkumbo.
Picha: Mauld Mmbaga
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Mipango na Uwekezaji Prof. Kitila Mkumbo.

WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Rais Mipango na Uwekezaji Prof. Kitila Mkumbo amewataka wafanyabiashara kutoacha kutoa maoni ya mambo mazuri yaliyofanyika katika Dira ya Taifa ya Maendeleo 2025 bali wayabebe kwa ajili ya kujumuishwa kwenye Dira 2050.

Prof. Kitila ameyasema leo Januari 8, 2025 katika mkutano wa wafanyabiashara na wamiliki wa kampuni wa kuhakiki rasimu ya Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050 unaofanyika Jijini Dar es Salaam.

Amesema mambo mazuri ambayo yametumika kwenye dira inayoisha muda wake ya mwaka 2000- 2025  yachukuliwe kama msingi wa kuelekea mbele.

"Kama kuna vitu tumevifanya kwa uzuri na tungetamani kuvibeba kwa ajili ya dira 2050 kama msingi wa miaka 25 ijayo lakini kitu kingine ni lazima kuacha mambo ambayo hayakuwa mazuri na ambayo hayakuonekana kuleta matunda kwa miaka 25 iliyopita," amesema Prof. Kitila.

Aidha, ameomba wafanyabiashara kuwa mstari wa mbele katika kuhakikisha Pato la Taifa na pato la mtu mmoja mmoja linaendelea kukua kwa kuwa wao ndio wameshika usukani wa kitaaluma katika sekta hiyo, wakitambua fursa na changamoto zake.

1