Rais Samia amtuza Mhariri Mtendaji Gazeti la Nipashe

By Christina Mwakangale , Nipashe
Published at 01:31 PM Jun 18 2024
Rais Samia Suluhu Hassan

RAIS Samia Suluhu Hassan, ametambua ushindi wa Mhariri Mtendaji wa Gazeti la Nipashe, Beatrice Bandawe, baada ya kushinda Tuzo ya Uongozi kwenye Vyombo vya Habari 2024 barani Afrika, kwa mara ya kwanza nchini.

Amesema anawatambua Watanzania walioshinda tuzo za kimataifa, akiwamo Bandawe, na kwamba wanahabari nchini waendelee kufanya kazi hiyo, kwa kuwa wameaminiwa na wanaiheshimisha Tanzania.

“Naomba niwatambue wachache ambao baadhi yao wako hapa…kwanza Beatrice Bandawe, aliyepata tuzo ya mwanamke kiongozi katika chombo cha habari WAN IFRA ambayo ni mara ya kwanza.. alisema Rais Samia.

Bandawe, ni Mhariri Mtendaji wa gazeti la Nipashe, linalochapishwa na kampuni ya The Guardian, alituzwa tuzo hiyo, ambayo hutolewa na Jumuiya ya Wachapishaji Duniani (WAN IFRA).

Mhariri Mtendaji wa Gazeti la Nipashe, Beatrice Bandawe, alipokabidhiwa tuzo hiyo hivi karibuni.