"Tanzania imekuwa kitovu cha amani na mshikamano wa kijamii barani Afrika na duniani kote", amesema Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres
"Tanzania kama ishara ya Amani ilijaribiwa katika uchaguzi wa hivi karibuni uliofanyika Oktoba 29, 2025 lakini nchi hii ilifanikiwa kupitia mtihani wa kwanza kabisa."
“Umoja wa Mataifa ungependa kuona Tanzania ikibaki kuwa na umoja na mfano mzuri”. Amesema Guterres, wakati akimpokea Mjumbe Maalum mwenye Ujumbe kutoka kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. Samia Suluhu Hassan, uliotolewa na Waziri wa Mambo ya Nje wa Tanzania Balozi Mahmoud Kombo.
Baraza la Umoja wa Mataifa (UNSG) lilisisitiza hitaji la mazungumzo ya kitaifa yenye maana na jumuishi ili kushughulikia sababu kuu za matukio ya vurugu ya Oktoba 29 yaliyotokea na njia za kuyashughulikia, ili kuzuia kujirudia kwake.”
Pia aliahidi Umoja wa Mataifa kuunga mkono kikamilifu na baada ya Tume ya Uchunguzi iliyoundwa nchini Tanzania kukamilisha jukumu lake.
© 2025 IPPMEDIA.COM. ALL RIGHTS RESERVED