PSSSF yapata tuzo banda bora maonesho ya 11 ya Kimataifa ya Biashara Pemba

By Mwandishi Wetu , Nipashe
Published at 11:51 AM Jan 10 2025
PSSSF yapata tuzo banda bora maonesho ya 11 ya Kimataifa  ya Biashara Pemba.
Picha:Mpigapicha Wetu
PSSSF yapata tuzo banda bora maonesho ya 11 ya Kimataifa ya Biashara Pemba.

MFUKO wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF) umepata Tuzo ya Banda Bora katika Maonesho ya 11 ya Kimataifa ya Biashara yanayofanyika kwa mara ya kwanza kwenye Kituo cha Maonesho Chamanangwe, Kisiwani Pemba.

Maonesho hayo ambayo ni sehemu ya shamrashamra za kuelekea sherehe za Mapinduzi ya Zanzibar yanayoadhimishwa Januari 12 kila mwaka, yameandaliwa na Wizara ya Biashara na Maendeleo ya Viwanda Zanzibar ili kutoa fursa kwa Taasisi za Serekali na za binafsi pamoja na Wajasiriliamali kuonesha, kutangaza na kuuza bidhaa zao kwa Wananchi.

Akizindua maonesho hayo, Waziri wa Utalii na Mali Kale wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Mudrik Ramadhan Soraga ametembelea banda la PSSSF ambapo Afisa Uhusiano wa PSSSF, Queen Edward amemfahamisha kuwa huduma za Mfuko zinapatikana katika ofisi zilizopo nchini nzima ikiwa ni pamoja na Unguja na Pemba. Kilele cha maonesho hayo ni Januari 15, 2025.