Mjumbe serikali ya kijiji auawa na mume kwa kukatwa na shoka kichwani

By Nebart Msokwa , Nipashe
Published at 06:02 PM Jul 03 2025
Mjumbe serikali ya kijiji auawa na mume kwa kukatwa na shoka kichwani

Mjumbe wa Serikali ya Kijiji cha Inyala katika Halmashauri ya Wilaya ya Mbeya, Neema Nsimama ameuawa kwa kukatwa na shoka kichwani na mumewe aitwaye Julius Paulo kwa kile kinachodaiwa kuwa ni kutokana na wivu wa mapenzi.