Wakati watia nia kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) katika mkoa wa Geita wakijitokeza kwa wingi kuchukua na kurejesha fomu za kuomba ridhaa ya kugombea ubunge, Jimbo la Bukombe limebaki na jina moja pekee—Naibu Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Doto Biteko, ambaye ameonesha nia ya kuendelea kulitumikia jimbo hilo.
Kwa mujibu wa takwimu zilizotolewa na Katibu wa Itikadi, Siasa na Uenezi wa CCM Mkoa wa Geita, Andrew Mnuke, jumla ya wanachama 102 wamejitokeza kuwania nafasi ya ubunge katika majimbo tisa ya mkoa huo. Hii ni dalili ya hamasa kubwa ya kisiasa kuelekea uchaguzi mkuu ujao na kuendelea kuimarika kwa demokrasia ndani ya chama hicho tawala.
Majimbo na idadi ya watia nia waliopokea fomu ni kama ifuatavyo:
Katika orodha hiyo, wanaume ni 85 na wanawake 17, jambo linaloashiria uhamasishaji unaoendelea kwa jinsia zote kushiriki kwenye uongozi wa taifa.
Akizungumza na waandishi wa habari, Mnuke amesema:
"Mwitikio huu mkubwa unaonyesha imani ya wanachama kwa chama chao na ari ya kushiriki kwenye mchakato wa demokrasia kuelekea uchaguzi mkuu. Hili ni jambo la kujivunia kama chama na kama mkoa."
© 2025 IPPMEDIA.COM. ALL RIGHTS RESERVED