Serikali yaanza kutekeleza chanjo ya mifugo Dar

By Thobias Mwanakatwe , Nipashe
Published at 07:28 PM Jul 03 2025
Serikali yaanza kutekeleza  chanjo ya mifugo Dar
Picha:Mpigapicha Wetu
Serikali yaanza kutekeleza chanjo ya mifugo Dar

Serikali imeanza kutekeleza Kampeni ya Chanjo ya Mifugo na Utambuzi Kitaifa kwa kuweka ruzuku ya asilimia 100 kwa chanjo za kuku ambazo zitatolewa bila malipo, asilimia 50 kwa chanjo za ng’ombe, mbuzi na kondoo ili kutokomeza magonjwa matano ya kipaumbele ya mifugo na kuimarisha biashara ya Mifugo na mazao yake.

Akizindua Kampeni hiyo kwa Mkoa wa Dar es Salaam leo 3 Julai, 2025 Katibu Mkuu wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi Agness Meena  amesema  mpango huo wa uchanjaji na utambuzi wa mifugo Kitaifa unaanza kutekelezwa katika mwaka wa fedha 2024-2025  ambapo shilingi bilioni 69.2 zimetengwa na serikali  kwa ajili ya  kufanikisha  Kampeni hiyo nchini.


" Tumeanza Kampeni yetu ya Chanjo na kwa ukanda wa huu wa Pwani tumeanza na Dar es Salaam katika shamba la mfugaji wetu la Zoo  hapa Kigamboni, ambapo zaidi ya Mifugo 200 inachanjwa leo , Serikali itagharamia shilingi 500 na mfugaji kuchangia shilingi 500 kwa chanjo ya ngo’mbe , shilingi 300 kwa chanjo ya mbuzi na Kondoo na mfugaji kuchangia shilingi 300 na chanjo ya kuku itatolewa bure" amesema  Meena.