TANZANIA imeanza rasmi kuzalisha baruti na vilipuzi, baada ya Kampuni ya Solar Group kuzindua kiwanda cha kuzalisha bidhaa hizo, wilayani Kisarawe mkoani Pwani.
Kiwanda hicho cha Solar Nitrochemicals, kimezinduliwa leo na Waziri wa Madini, Antony Mavunde, amesema kiwanda hicho kina uwezo wa kuzalisha tani 22,000 za baruti na vipuli milioni 15 kwa mwaka.
"Tunalenga kukidhi mahitaji ya ndani na kusambaza bidhaa katika masoko ya Afrika Mashariki na Kusini,Tunaendelea kuwekeza kwa ajili ya ukuaji mkubwa hadi mwaka 2030, tunashukuru sana kwa mwongozo na usaidizi wa serikali, " amesema Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni hiyo, Milind Deshmukh.
Amesema wamefanya uwekezaji wa Sh. bilioni 19 na kitakuwa na uwezo wa kuajiri Watanzania 300 na kwamba lengo ni kuhudumia ukanda wa Afrika Mshariki na Kusini.
© 2025 IPPMEDIA.COM. ALL RIGHTS RESERVED