MAMLAKA ya Udhibiti Usafiri Ardhini(LATRA), imesema mwisho wa mwezi huu itatoa taarifa ya utekelezaji wa mifumo ya tiketi mtandao na hatua mbalimbali inazozichukua za udhibiti kwenye eneo hilo.
Kadhalika, imetoa taarifa kuhusu kampuni ambazo zimefanya vizuri katika eneo hilo.
Kwa mujibu wa taarifa ya Mkuu wa Kitengo cha Uhusiano na Mawasiliano wa LATRA, Salum Pazzy, hadi Julai 19 mwaka huu, idadi ya kampuni zilizokidhi vigezo vya kupata vibali vya kutoa huduma za tiketi mtandao ni tano.
Kadhalika, amesema kampuni nyingine nne ambazo zimeonesha mwelekeo mzuri, bado zinaendelea kukamilisha taratibu kwa mujibu wa sheria.
"LATRA imeridhika na juhudi zao na inaendelea kuwasaidia ili kuhakikisha zinakamilisha taratibu za kusajiliwa mapema,"amesema Pazzy.
Pia, amesema kampuni nyingine mbili ambazo awali zilibainika kuwa na changamoto kadhaa na kupewa siku saba za matazamio kuhakikisha zinakamilisha matakwa ya kisheria, kwa sasa zimeonesha mwelekeo mzuri na zimepewa muda kukamilisha.
© 2025 IPPMEDIA.COM. ALL RIGHTS RESERVED