TEF yashuhudia zao parachichi linavyoinua mkulima

By Mwandishi Wetu , Nipashe Jumapili
Published at 05:16 PM Apr 06 2025
TEFlimetembelea kiwanda cha kuchakata mafuta ya parachichi
Picha: Elizabeth John
TEFlimetembelea kiwanda cha kuchakata mafuta ya parachichi

JUKWAA la Wahariri (TEF), limetembelea kiwanda cha kuchakata mafuta ya parachichi, Avo Africa kilichopo kijiji cha Mtewele, wilayani Wanging'ombe mkoa wa Njombe.

Akizungumza leo, Aprili 6, 2025, mara baada ya kutembelea kiwanda hicho, Mwenyekiti wa TEF, Deodatus Balile, amesema uwapo wa kiwanda hicho ni mkombozi mkubwa kwa wakulima.

"Naona sasa kuna juhudi kubwa ya watu kuanzishiwa viwanda, kulima mashamba kufanya kila kitu ambacho kinawezekana kuwaondoa katika umasikini, jambo lililotokea hapa kwamba maparachichi yaliyokuwa ‘reject’ leo yananunuliwa kwa Sh. 750 ni mkombozi mkubwa kwa mkulima wa kawaida," amesema Balile.

TEF limetembelea kiwanda cha kuchakata mafuta ya parachichi
Ameupongeza uongozi wa mkoa wa Njombe kwa kutafsiri kwa vitendo maelekezo ya Rais Samia Suluhu Hassan na kwamba jambo hilo litasaidia nchi kutoka ilipo sasa.
TEFlimetembelea kiwanda cha kuchakata mafuta ya parachichi
Mkuu wa Wilaya ya Wanging'ombe, Zakaria Mwansasu, kwa niaba ya Mkuu wa mkoa huo, Anthony Mtaka, amesema uwapo wa viwanda hivyo umewarahisisha kuwahamasisha wakulima kuzalisha zaidi tofauti ya huko nyuma, ambako kulikuwa hakuna njia mbadala.