JUMLA ya wagombea 23 wa vyama vya siasa wamechukua fomu za kuwania ubunge katika majimbo ya Mtumba na Dodoma Mjini, mkoani hapa katika Uchaguzi Mkuu utakaofanyika nchini Oktoba 29, mwaka huu.
Uchaguzi huo wa rais, wabunge na madiwani utakaovishirikisha vyama vingi vya siasa nchini, unafanyika kwa mujibu wa ratiba ya Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC). Akizungumza na Msimamizi wa Uchaguzi Jimbo la Dodoma Mjini, Wakili Cosmas Msemwa amesema kuwa mpaka sasa wagombea hao, wamechukua fomu hizo na kwamba idadi inaweza kuongezeka kutokana na watia nia wengine kuendelea kujitokeza.
Alivitaja vyama vilivyoongezeka baada ya wagombea hao kujitokeza katika Jimbo la Dodoma Mjini ni CCK,naTLP (Jimbo la Dodoma mjini),wakati Jimbo la Mtumba waliongezeka ni TLP,UDP na CIF
Vyama vilivyochukua awali na majimbo yao ni Chama Cha Wananchi (CUF), Union for Multiparty Democracy (UMD) , Chama Cha Kijamii (CCK) na Chama Makini (MAKINI). Vingine kwa upande wa Jimbo la Mtumba ni United People Democratic Party (UDPD), Alliance for African Farmers Party (AAFP) na African Democratic Alliance Party (ADA TADEA).
Vingine ni Sauti ya Umma (SAU), Democratic Party (DP), The National League For Democratic (NLD),NRA na Makini. Kwa upande wa Jimbo la Dodoma wagombea sita waliochukua fomu hizo ni wa United People Democratic Party (UPDP), AAFP, ADA TADEA, SAU, NLD na MAKINI.
Wakili Msemwa amesema kwa upande wa Madiwani vyama vilivyochukua fomu katika Kata ya Majengo ni UPDP, Kata ya Madukani UPDP, Majengo CUF, Madukani ACT Wazalendo, Kizota DP, na Ipala ADA TADEA.
© 2025 IPPMEDIA.COM. ALL RIGHTS RESERVED