Wakiwa eneo la Kisaki, Mkoani Pwani, Mgombea urais kwa tiketi ya AAFP, Kunje Ngombale Mwiru amesema serikali yake itakuwa ya kwanza kunyonga mafisadi ambao atawanyonge hadharani na kwamba lazima mipaka yote ifingwe wasikimbie.
"Tarehe 29, 2025 nitakuwa mtu wa kwanza kunyonga watu, nitakuwa mtu wa kwanza katika nchi za Afrika kunyong’a mafisadi, wanaojulikana ni mafisadi nitaongea na Idara ya Usalama wa Taifa mipaka ifungwe mafisadi wote wakamatwe na wanyongwe.
“Leo fisadi amekula fedha ya zahanati tatu alafu uamuona anatamba mjini, mimi mwenyewe nitashuhudia akinyongwa, mtu kafanya ufisadi kala fedha ya shule tatu, zahanati alafu leo mnatamba naye mtaani, sasa twende na mmoja fisadi anayekula fedha za umma au twende na wengi?alihoji huku akitaka wananchi wanaounga mkono hoja yake wanyooshe mikono.
Alisema atajadiliana na Jaji atakayemteua ili mafisadi wote wahukumiwe kunyongwa, “Nichagueni ili muone kama mipaka yote haijafungwa tarehe 29, ili tuwakamate mafisadi wote.”
© 2025 IPPMEDIA.COM. ALL RIGHTS RESERVED