Samia: Tatizo la maji Dodoma kuwa historia

By Romana Mallya , Nipashe Jumapili
Published at 07:05 PM Aug 31 2025
Mgombea urais CCM, Samia Suluhu Hassan
PICHA: CCM
Mgombea urais CCM, Samia Suluhu Hassan

Mgombea urais CCM, Samia Suluhu Hassan, ametaja moja ya ahadi kwa jiji la Dodoma endapo atapata ridhaa tena kuongoza nchi atakwenda kumaliza tatizo la maji pamoja na migogoro ya ardhi.

Ametoa kauli hiyo leo Agosti 31, 2025, katika mkutano wa kampeni uliofanyika uwanja wa Tambukareli, Dodoma, ukihudhuriwa na maelfu ya wnanachi. Amesema chama kimejipanga kumaliza tatizo la maji mji wa Dodoma kupitia mradi mkubwa kutoa maji Ziwa Victoria, kwa sababu ndio Makao Makuu ya nchi.

Jambo lingine aliloahidi ni kuongeza kasi ya upimaji ardhI ili kumaliza migogoro itokanayo na hilo na pia watavutia uwekezaji mkubwa wa viwanda na uongezaji thamani. “Umeme wakati mwingine ni mdogo au unakatikakatika  tunajenga njia kutoka Chalinze-Dodoma kupata umeme kilovoti 400 ili shughuli zote zifanyike zikiwamo za viwanda,” amesema.