Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU), Mkoa wa Kilimanjaro, imeokoa Sh.136,583,458 katika mradi wa ujenzi wa shule mpya ya Sekondari Hedaru, Wilaya ya Same,ambazo zilitumika bila kukata kodi ya zuio.
Kwa mujibu wa Mkuu wa TAKUKURU, mkoani humo, Mussa Chaulo, gharama za ujenzi wa mradi huo ni Sh. 586,170,029.
Amesema katika ufuatiliaji huo, ilibainika kuwa Sh. 136,583,458 zimetumika bila kukata kodi ya zuio, kiasi cha kodi ambacho kilichopaswa kulipwa ni Sh. 9,970,592.43
Aidha, Chaulo, amesema baada ya kubaini hilo, TAKUKURU Wilaya ya Same, ilimuandikia barua Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya hiyo, ikimtaka kukatwa na kuwasilishwa kwa kodi husika kwa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA).
"Mnamo Mei 2025, kiasi chote cha shilingi 9,970,592.43 kilikatwa na kuwasilishwa TRA,"amesema.
© 2025 IPPMEDIA.COM. ALL RIGHTS RESERVED