KATIKA kipindi cha miaka mitano ijayo Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimeahidi kupeleka mabadiliko ya kimaendeleo wilayani Rorya mkoani Mara, ikiwemo kufikisha umeme katika vitongoji vyote.
Pia, kimeahidi kujenga vituo vya afya vya kisasa vitano vitakavyokuwa na uwezo wa kutoa huduma za kibingwa, pamoja na ujenzi wa zahanati 10. Mgombea Mwenza wa Urais wa CCM, Dk. Emmanuel Nchimbi alitoa ahadi hizo leo wakati akiwahutubia wananchi wa Rorya. Ikiwa ni mwendelezo wa kampeni za Uchaguzi Mkuu wa Rais, Wabunge na Madiwani.
Dk. Nchimbi alisema: "Katika miaka mitano ijayo tutaajiri watumishi wa afya 150. Ujenzi wa Chuo cha Veta utakamilika. Shule za sekondari 10 na msingi tano zitajengwa hapa Rorya. Pia idadi ya majosho itafikia 19. Vizimba vya samaki vitafikia 43".
© 2025 IPPMEDIA.COM. ALL RIGHTS RESERVED