WAKATI kampeni za Uchaguzi Mkuu zikiingia siku ya nne leo, Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimeahidi kuleta mabadiliko katika sekta ya afya, elimu na miundombinu katika miaka mitano ijayo Tarime Vijijini.
Akizungumza leo Agosti 31 na wakazi wa Nyamongo, Mgombea Mwenza wa Urais wa chama hicho, Dk. Emmanuel Nchimbi amesema miaka mitano ijayo endapo chama hicho kikishinda katika Uchaguzi Mkuu kitaleta mageuzi makubwa Tarime Vijijini.
Dk. Nchimbi aliyataja mambo watakayoyatekeleza ni kuongeza idadi ya zahanati zifike 70, vituo vya afya vifike 20, idadi ya watu wanaopata huduma ya majisafi na salama iongezeke na iwe kati ya wananchi 100, wananchi 95 wawe na uhakika wa kupata huduma hiyo.
Dk. Nchimbi alisema mipango mingine ni ujenzi wa barabara za lami ambazo ni Barabara ya Tarime hadi Mgumu (km87), Barabara ya Mogabiri hadi Nyamongo (km 25), Barabara ya Tarime hadi Mogabiri (km 93) pamoja na Barabara ya Nyamongo hadi Mgumu (km 48).
© 2025 IPPMEDIA.COM. ALL RIGHTS RESERVED