Vituo malezi 12, bababora, mamalishe 100 wapatiwa mitungi ya gesi

By Hellen Mwango , Nipashe Jumapili
Published at 02:28 PM Aug 31 2025
Askofu wa Kanisa la Ufunuo (The Revelation Church Tanzania), Yaspi Bendera
Picha: Hellen Mwango
Askofu wa Kanisa la Ufunuo (The Revelation Church Tanzania), Yaspi Bendera

VITUO 12 vinavyolea watoto wenye mazingira magumu, mama lishe zaidi ya 100 na baba bora 20 wa Mkoa wa Dar es Salaam, wamekabidhiwa majiko na mitungi ya gesi yenye thamani ya Sh. milioni 2.6.

Tukio hilo limefanyika katika tamasha la nane la Mama Lishe, Baba Bora na Mtoto Kwanza, jijini Dar es Salaam.

Akizungumza kwenye tamasha Hilo, Mrakibu Msaidizi wa Polisi (ASP), Blandina Ndunguru kutoka Dawati la Jinsia Mkoa wa Kipolisi Temeke, amesema ukatili na unyanyasaji wa kimwili unaomsababishia maumivu ya kimwili na kihisia kwa watoto, umefika hatua mbaya kwa sababu ya malezi mabovu ya wazazi.

Ameitoa witoa kwa wazazi nchini kushirikia kikamilifu malezi ya watoto, ikiwamo kuwapa muda wa kuzungumza nao, ili kupunguza watoto wanaoishi kwenye mazingira magumu na ukatili dhidi yao.

“Wanawake tunafeli kulea watoto wetu tunawaza kausha damu, tunasababisha unyanyasaji kwa watoto tuwalinde, tuwasilikize, tuache kufanya watoto mtaji.

“Mtoto akibakwa au kulawitiwa tuache kuwafanya mtaji na kukubali kupokea pesa fikisheni kwenye vyombo vya sheria badala ya kumalizana mtaani au kusamehe, kwa sababu aliyefanya ukatili husika ni ndugu au mwanafamilia, wote ni lazima wafikishwe kwenye mkono wa sheria,” amesema Ndunguru.

Akifafanua zaidi alisema wazazi washirikiane katika malezi, upelelezi wa masuala yanayohusu ukatili wa watoto, pamoja na kuepuka tabia ya kuwalaza watoto na wageni wanaowatembelea majumbani mwao.

Rais wa Mama Lishe nchini, Latifa Masasi, amesema lengo la tamasha hilo ni kuwaweka Pamoja mama lishe ikiwamo kutoa elimu kuhusu malezi na kupunguza yatima mitaani, unyanyasaji na ukatili dhidi ya watoto.

Amesema wazazi wote wana majukumu sawa katika malezi ya watoto na kwamba wapo wanaume wanaoshiriki kikamilifu katika malezi na wanawatambua kama baba bora.

Yusuph Kadi, mkazi wa Mbagala ni baba bora anayeisaidia familia yake katika majukumu yote, ikiwamo kufua, kuosha vyombo, kupeleka mtoto kliniki pamoja na kuwapa muda wa kuongea nao watoto wake, alitajwa baba bora anayeshiriki malezi ya watoto wake kwa asilimia mia moja.

Askofu wa Kanisa la Ufunuo (The Revelation Church Tanzania), Yaspi Bendera, ameema wanawake waamke katika ujenzi wa familia ikiwamo katika ujasiriamali na ujuzi wa masuala yote yanayokuza uchumi wa familia.

“Mimi pamoja na kuwa askofu lakini ni mjasiriamali kwa hiyo wanawake tuamke, wajane muunde vikundi niko tayari kuja kutoa elimu bure ya ujasiriamali ili mkue kiuchumi na kumudu kutunza familia.