CHADEMA Zanzibar kama bara

By Rahma Suleiman , Nipashe Jumapili
Published at 07:05 PM Aug 24 2025
CHADEMA
PICHA: MTANDAO
CHADEMA

CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) – Zanzibar kimesema kuwa kimeamua kutoshiriki na kutosaini maadili hayo kutokana na msimamo wetu wa muda mrefu kwamba hakutakuwa na uchaguzi huru, wa haki na wenye kuaminika Zanzibar bila kufanyika kwanza mageuzi ya kisheria na kikatiba (Electoral Reforms).

Akitoa taarifa kwa vyombo vya habari Mkuu wa  Idara ya Habari Uenezi na Mawasiliano kwa Umma wa chama hicho, Zanzibar Hamad Mussa Yussuf,amesema maadili ya Uchaguzi si mbadala wa mageuzi ya kweli.

“Hati hii iliyosainiwa leo ni ya kifomu (cosmetic) na inalenga kuhalalisha mchakato batili. Haki za wananchi haziwezi kulindwa kwa maadili yasiyo na nguvu za kisheria wala dhamira ya kisiasa”amesema.

Hamad amesema hakuna marekebisho ya sheria za uchaguzi licha ya maombi ya wadau, Serikali imekataa kurekebisha sheria kandamizi za uchaguzi ambazo zinatoa mamlaka makubwa kwa ZEC bila uwazi wala uwajibikaji.

“Msimamo wetu ni NO REFORMS, NO ELECTION – Tunasisitiza msimamo huu si kwa faida ya chama pekee bali kwa mustakabali wa Zanzibar yenye haki, amani, demokrasia na maridhiano ya kweli”amesema.

Aliwataka wananchi wote wa Zanzibar kutambua kwamba kushiriki katika uchaguzi usio na mageuzi ni kuhalalisha udhalimu na kudumaza demokrasia.