CHAUMMA: Tutawaondoa wanawake kwenye 'kausha damu'

By Christina Mwakangale , Nipashe Jumapili
Published at 04:30 PM Aug 10 2025
Makamu Mwenyekiti wa CHAUMMA, Devotha Minja (kushoto), akiwa na Agnesta Kaiza, mgombea ubunge wa jimbo hilo
Picha: Christina Mwakangale
Makamu Mwenyekiti wa CHAUMMA, Devotha Minja (kushoto), akiwa na Agnesta Kaiza, mgombea ubunge wa jimbo hilo

WANAWAKE wa Jimbo la Segerea, wametakiwa kutumia haki yao ya kikatiba, kwa kupiga kura Oktoba 29, mwaka huu, ili kuleta mabadiliko kijamii.

Mgombea mwenza wa nafasi ya urais, Chama cha Ukombozi wa Umma (CHAUMMA), Devotha Minja, amesema hayo leo, Agosti 09, 2025, kwanye kongamano la wanawake wa chama hicho jimbo hilo, lililofanyika Tabata, Dar es Salaam.

“Mabadiliko yatatokanana na ninyi. Hali hii ilivyo, kinamama wamechoka, hamna matumaini, furaha, kwa sababu mna mbunge wa CCM. Sababu mbunge wenu hashughulikii matatizo yenu wanawake.


“Kuna mikopo inayotolewa na halmashauri ya asilimia 10, kwa vijana, wanawake na watu wenye ulemavu lakini hampati mikopo hiyo. Wanapeana wao wenyewe. CHAUMMA itawakomboa wanawake, muachane na mikopo ‘kausha damu’.

Minja, ambaye pia ni Makamu Mwenyekiti wa chama hicho bara, amesema kwamba mabadiliko ya aletwa na CHAUMMA, mwaka huu, kwa kuipumzisha CCM,” amesema. 

Wanawake wa CHAUMMA kwenye kongamano hilo, jana
Agnesta Kaiza, mgombea ubunge wa jimbo hilo, kupitia CHAUMMA, amesema barabara mbovu jimboni humo zimewaathiri zaidi wanawake.

“Wanawake wa Segerea viuno viko hoi, sababu ya barabara mbovu. Mbunge yupo. CCM mikopo wanaitoa wao kwa wao, akinamama wengine wamechoshwa na kausha damu,” amesema na kuongeza:

“Kama mwanamke nasema haiwezekani wanyanyasike fedha zao zipo.”

Jimbo la Segerea, likiwa miongoni mwa yaliyoko mkoani Dar es Salaam, Iina kata 13 na mitaa 61.