MKURUGENZI wa Rasilimali wWatu wa Chama cha Ukombozi wa Umma (CHAUMMA), Khadija Mwago, amechukua fomu ya kutia nia ya Ubunge jimbo la Mbagala.
"Nimesimama nikiwa na nia na dhamira ya kwenda kuwatumikia wananchi wa Mbagala, safafi hii tunawaambia tumedhamiria kushinda jimbo hili.
“Tunakwenda kuwachezesha ngoma CCM mpaka tuhakikishe tumechimba, aidha wametaka au hawajataka safari hii tunataka mabadiliko."
"Ninakwenda kusimama kuwa sauti ya wana-Mbagala, ninakwena kupigania upatikanaji wa mikopo isiyo na riba na kukomesha mikopo ya kausha damu.
“Ninakwenda kupigania fursa ambazo zimeshindwa kupatikana kwa muda mrefu Mbagala."
© 2025 IPPMEDIA.COM. ALL RIGHTS RESERVED