CHAMA cha Mapinduzi (CCM) kimesema hadi sasa hakuna aliyekatwa, kufyekwa au kuenguliwa katika mchakato wa uteuzi wa wagombea wa ubunge, uwakilishi na udiwani hadi pale Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya chama hicho itakapokamilisha kazi yake.
Katibu wa NEC Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa CCM, Amos Makalla ameyasema hayo leo jijini Dodoma alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari kuhusu kuanza kwa vikao vya CCM ngazi ya Taifa.
Makalla amewaasa watia nia kuwa watulivu katika kipindi hiki ambacho mchakato bado unaendelea hadi pale Kamati kuu itakapotoa uamuzi wa mwisho.
"Mchakato wa nani kateuliwa, nani hajateuliwa bado haujaisha hadi kamati kuu itakapokamilisha kazi yake ya kuteua majina ya wagombea watakaopigiwa kura za maoni.
"Kama mnavyojua nafasi ni chache kulingana na idadi ya walioomba, hata ambao hawatateuliwa chama kinawathamini watia nia wote na waendelee kuwa watulivu kwa chama chao,"amesema.
© 2025 IPPMEDIA.COM. ALL RIGHTS RESERVED