Mgombea wa nafasi ya urais kupitia Chama cha Maarifa, Kilimo na Nishati (Makini), Coaster Kibonde, ametaja vipaumbele vitatu vya serikali yake endapo atashinda Uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba mwaka huu.
Kibonde amewasili leo Agosti 10, 2025, majira ya saa 9:09 alasiri katika ofisi za Tume Huru ya Uchaguzi (INEC) zilizopo Njedengwa, Jijini Dodoma, akiwa na mgombea mwenza wake pamoja na wanachama wa chama hicho, kwa ajili ya kuchukua fomu ya kugombea nafasi ya Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Akitaja vipaumbele hivyo, Kibonde amesema vitahusisha sekta za Elimu, Afya, na Kilimo:
Kibonde amesema utekelezaji wa vipaumbele hivyo utalenga kuhakikisha kila raia anapata haki yake katika huduma za kijamii na kiuchumi.
Aidha, leo vyama vitatu vya siasa vinatarajiwa kuchukua fomu za kugombea nafasi ya Urais katika ofisi za INEC, Jijini Dodoma.
© 2025 IPPMEDIA.COM. ALL RIGHTS RESERVED