Mwenge wa Uhuru watua Shinyanga

By Marco Maduhu , Nipashe Jumapili
Published at 04:27 PM Aug 03 2025
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Mboni Mhita (kulia), akipokea Mwenge wa Uhuru kutoka kwa Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Paul Chacha
Picha: Marco Maduhu
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Mboni Mhita (kulia), akipokea Mwenge wa Uhuru kutoka kwa Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Paul Chacha

MKUU wa Mkoa wa Shinyanga, Mboni Mhita, amepokea Mbio za Mwenge wa Uhuru kutoka kwa Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Paul Chacha.

Amepokea Mwenge huo, leo, Agosti 3, 2025 katika Viwanja wa Stendi ya Mabasi Kagongwa, wilayani Kahama.

Amesema Mwenge huo wa Uhuru ukiwa Mkoani Shinyanga utakimbizwa umbali wa kilomita 819.2 ndani ya Hhalmashauri sita na kupita katika miradi 44 kukagua,kuzindua na kuweka Mawe ya Msingi miradi ya Sh. bilioni 17.3

Mbio hizo za Mwenge wa Uhuru, unakimbizwa na wakimbiza Mwenge sita, wakiongozwa na kiongozi Ismail Ali Ussi.

Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Mboni Mhita (kulia), akipokea Mwenge wa Uhuru kutoka kwa Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Paul Chacha

Kauli Mbiu ya Mwenge wa Uhuru mwaka huu inasema," Jitokeze kushiriki uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2025 kwa Amani na Utulivu.

Mwenge huo utakabidhiwa mkoani Simiyu, Agost 9, 2025.