Serikali kutoa mwongozo kima cha chini mshahara sekta binafsi

By Christina Mwakangale , Nipashe Jumapili
Published at 06:31 PM Aug 17 2025
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Ajira  Vijana na Watu wenye Ulemavu, Ridhiwani Kikwete
Picha: Mpigapicha Wetu
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Ajira Vijana na Watu wenye Ulemavu, Ridhiwani Kikwete

SERIKALI imesema hivi karibuni inatarajia kusaini Sheria ya Mwongozo wa Kima cha Chini cha Mshahara kwa Taasisi za Sekta Binafsi, zinazofanya kazi nchini.

Imesema katika mwongozo huo unatarajia kuainisha viwango vipya vya mshahara, kwa wafanyakazi wa sekta binafsi kulipwa.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Ajira  Vijana na Watu wenye Ulemavu, Ridhiwani Kikwete amesema hayo mwishoni mwa wiki, jijini Arusha.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Ajira Vijana na Watu wenye Ulemavu, Ridhiwani Kikwete (kushoto), akiteta jambo
Amesema mazungumzo yameshafanyika baina ya wadau ambao ni taasisi binafsi na wasimamizi wa sera lakini pia uongozi wa timu ya wizara, iliyopewa jukumu la kusimamia marekebisho hayo, na huenda viwango vilivyowekwa na kuanza mapema mwezi ujao.