VYAMA 18 vimejitokeza kushiriki kusaini kanuni za maadili ya Uchaguzi Zanzibar mwaka 2025 huku Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA kikisusia kusaini kanunuzi hizo za maadili.
Kusainiwa kwa maadili hayo ni kiashiria rasmi cha kuanza mchakato wa uchaguzi mkuu wa Oktoba 29 mwaka huu ambapo ZEC itafungua dirisha lake la uchukuaji wa Fomu Agosti 28 mwaka huu .
Hafla hiyo ya utiaji saini ilifanyika leo katika Ofisi za ZEC Maisara Mjini Zanzibar na kuhudhuriwa na wadau wa uchaguzi wakiwemo wanasiasa kutoka vyama mbalimbali. Vyama 18 vilivyosaini kanuni hizo ni Chama cha AAFP,ADC,ACT Wazalendo,CCM,ADA TADEA,CHAUMA,CUF,DP,CCK,MAKINI,NCCR Mageuzi,NLD,NRA,TLP,SAU,UDP,ULD,UPDP.
Akizungumza katika hafla hiyo Mwenyekiti wa ZEC, Jaji George Joseph Kazi alisema kifungu cha 65 ya uchaguzi namba 4 ya mwaka 2018 kinaiyelekeza tume kwa kushirikiana na vyama vya siasa,mrajisi wa vyama vya siasa na mamlaka za serikali kutayarisha kanuni za maadili kuongoza shughuli za vyama na wadau wengine wa uchaguzi.
Amesema kanuni hizo zitatumika katika uchaguzi wa mwaka huu, na kuwataka kila wadau ambapo vyama vya siasa wanawajibu kulinda hali ya usalama,utulivu na amani ya Zanzibar.
© 2025 IPPMEDIA.COM. ALL RIGHTS RESERVED