Andengenye amkabidhi Sirro jukumu lake

By Adela Madyane , Nipashe
Published at 05:10 PM Jul 03 2025
Andengenye amkabidi Sirro jukumu lake
Picha: Mtandao
Andengenye amkabidi Sirro jukumu lake

ALIYEKUWA Mkuu wa Mkoa wa Kigoma, Thobias Andengenye, amekabidhi rasmi madaraka kwa mkuu mpya wa mkoa huo, Simon Sirro, katika hafla iliyofanyika Julai 2, 2025.

Hafla imehudhuriwa na viongozi wa wilaya, wakuu wa taasisi mbalimbali, wawakilishi wa serikali, viongozi wa vyama vya siasa pamoja na wananchi.

Andengenye ametoa shukrani kwa Rais Samia Suluhu Hassan, kwa imani aliyooneshwa kwake kwa kumteua kuongoza mkoa huo kwa kipindi cha miaka mitano.

Sirro ameeleza kuwa, moja ya maagizo aliyopewa ni kuhakikisha mkoa wa Kigoma unafunguliwa zaidi katika sekta za utalii, biashara na uwekezaji huku akitoa wito wa ushirikiano kwa wananchi, viongozi na watumishi wote wa mkoa.