DC apewa jukumu la kukamilisha miradi

By Shaban Njia , Nipashe
Published at 04:45 PM Jul 03 2025
Mkuu wa mkoa wa Shinyanga, Mboni Mhita, akimkabidhi nyaraka za ofisi Mkuu wa Wilaya ya Kahama, Frank Nkinda, wakati wa hafla ya makabidhiano ya ofisi.
Picha: Shaban Njia
Mkuu wa mkoa wa Shinyanga, Mboni Mhita, akimkabidhi nyaraka za ofisi Mkuu wa Wilaya ya Kahama, Frank Nkinda, wakati wa hafla ya makabidhiano ya ofisi.

MKUU wa Wilaya ya Kahama, Frank Nkinda, ametwishwa jukumu la kuhakikisha miradi ya maendeleo inayotekelezwa kwa fedha kutoka serikali kuu, inakamilika kwa wakati.

Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Mboni Mhita, kwenye makabidhiano ya Ofisi yaliyohudhuriwa na viongozi mbalimbali kutoka Halmashauri za Msalala, Ushetu na Manispaa ya Kahama, ameema miradi ni mingi na inatakiwa kukamilika kwa muda ulipangwa nasio vinginevyo.

Amesema, anawajibu wa kusikiliza na kutatua kero mbalimbali za wananchi hasa katika sekta ya afya, elimu, maji, kilimo na miundombinu ya barabara huku ile miradi ya maendeleo inayotekelezwa na fedha za serikali kuu inakamilika kwa wakati na kuanza kutoa huduma na watakaobainika kukwamisha asisite kuchukua hatua.

Pia amesema, kunamradi wa kongani ya biashara iliyopo kulipokuwa mgodi wa Barrick Buzwagi kata ya Mwendakulima manispaa ya kahama unaendelea na mpaka sasa kuna wawekezaji 15 na Mgodi wa Kabanga Nikeli nao hivi karibuni unakwenda kujenga kinu cha kuchenjua madini katika eneo hilo.

Mhita amesema, lengo kuu la kongani ya biashara ia kurudisha mzunguko wa fedha na uchumi uliowepo kwa wananchi pale mgodini walipokuwa ukifanyakazi, hivyo hautakiwi kukwama kwa aina yeyote ile kwani utakuja kuajiri vijana wengi na kuendesha maisha yao.

Mkuu wa Wilaya ya Kahama, Frank Nkinda (kulia), akisalimiana na Katibu wa Baraza la Wazee Manispaa ya Kahama Mzee Anderson Lymo, wakati wa hafla ya kumpokea na kumkabidhi ofisi
“Mradi hii ni baadhi kwani ipo mingi na yote inatakiwa kukamilika kwa wakati, sitaki kusikia mradi umekwama kwa sababu ya fadha kuisha na kama kunakiasi cha fedha kinahitajika ili kukamilisha, basi halmashauri husika itoe fedha sehemu ya mapato ya ndani, ili kutokupoteza mud awa utekelezaji wake,” mmeongeza Mhita.

Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Wwilaya hiyo, Thomas Muyonga, amesema mradi wa uboreshaji miundombinu ya miji Tanzania (TACTIC) wa ujenzi nwa barabara na taa zake, masoko ya kisasa pamoja na vituo vya basi unaendelea nao unahitaji kuongezewa msukomu ili ukamilike kwa wakati.

Mkuu wa wilaya hiyo, Frank Nkinda, ameahidi kuisimamia miradi yote na kuhakikisha inakamilika kwa wakati na kuanza kutoa huduma ikiwa ni pamoja na kusikiliza kero za wananchi wa halmashauri ya Msalala, Ushetu na Manispaa ya Kahama na kuzitafitia ufumbuzi wake na zile zitazokuwa nje ya uwezo wake ataziwasilisha kwake.