Serikali imewaita kazini walimu wapya 319 wa fani mbalimbali, ambapo halmashauri saba zimenufaika na kuongezewa nguvu kazi hiyo mpya katika sekta ya elimu.
Taarifa ya kuitwa kazini kwa walimu hao ilitolewa jana, Machi 12, 2025, na Katibu wa Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma.
Kwa mujibu wa taarifa hiyo, waombaji wa nafasi za ualimu waliofanya usaili kati ya Septemba 4, 2024, na Februari 24, 2025, wamepangiwa vituo vya kazi kulingana na matokeo yao.
"Katibu wa Sekretarieti ya Ajira anapenda kuwataarifu waombaji kazi wa nafasi mbalimbali waliofanya usaili kuwa matokeo ya waliofaulu yanaweza kupatikana kwenye tangazo hili. Orodha hiyo pia inajumuisha baadhi ya waombaji waliokuwepo kwenye kanzidata (Database) kwa kada mbalimbali, ambao sasa wamepangiwa vituo vya kazi baada ya nafasi kupatikana," inaeleza sehemu ya taarifa hiyo.
Walimu hao wamepangiwa kufanya kazi katika halmashauri zifuatazo:
✅ Halmashauri ya Manispaa ya Songea
✅ Halmashauri ya Manispaa ya Kahama
✅ Halmashauri ya Jiji la Arusha
✅ Halmashauri ya Manispaa ya Tabora
✅ Halmashauri ya Wilaya ya Iramba
✅ Halmashauri ya Wilaya ya Magu
✅ Halmashauri ya Wilaya ya Kaliua
© 2025 IPPMEDIA.COM. ALL RIGHTS RESERVED