Arsenal, Real Madrid (Me &Ke) kunyukana robo fainali UCL

By Vitus Audax , Nipashe
Published at 11:16 PM Mar 13 2025
Arsenal, Real Madrid (Me &Ke) kunyukana robo fainali UCL
Picha: Mtandao
Arsenal, Real Madrid (Me &Ke) kunyukana robo fainali UCL

TIMU za Real Madrid na Arsenal zinatarajia kumenyana katika robo fainali ya Ligi ya mabingwa barani Ulaya UEFA (UCL) kwa wanaume na wanawake.

Arsenal Wanawake wanatarajia kukutana mapema Machi 18,2025 na wababe hao Real Madrid Wanawake majira ya saa mbili usiku.

Timu hizo zitarudiana Machi 26,2025 majira ya saa tano kamili usiku ili kupata mshindi atakaye kipiga katika mchuano wa nusu fainali ya Ligi hiyo maarufu ulimwenguni.

Kadhalika timu ya Arsenal wanaume pamoja na Real Madrid Wanaume wanatarajia kunyukana April 8,2025 majira ya saa nne kamili usiku.

Aidha marudiano ya mtanange huo mkali yatakuwa Aprili 16, 2025 majira ya saa nne kamili usiku.