Mrithi wa Kinana kupatikana hivi karibuni

By Ibrahim Joseph , Nipashe
Published at 03:04 PM Jan 07 2025
Aliyekuwa Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM)-Bara, Abdulrahman Kinana.

Mrithi wa aliyekuwa Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM)-Bara, Abdulrahman Kinana anatarajiwa kupatikana katika Mkutano Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) unaotarajiwa kufanyika Januari 18 na 19, mwaka huu jijini Dodoma.

Katibu wa NEC Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa CCM Taifa, Amos Makalla, amesema hayo leo, Januari 7, jijini Dodoma, wakati wa mkutano wake na waandishi wa habari uliofanyika katika ukumbi wa Halmashauri Kuu ya CCM Makao Makuu.

Amesema nafasi hiyo ya Makamu Mwenyekiti Taifa, iliyoachwa wazi na Kinana, mrithi wake atachaguliwa na wajumbe wa Mkutano Mkuu huo unaotarajiwa kufanyika Januari 18 na 19 Dodoma.

Makalla amesema kabla ya Mkutano Mkuu, kutakuwa na vikao vya Kamati Kuu ya CCM vitakavyofanyika Januari 16, mwaka huu, kama sehemu ya maandalizi ya Mkutano Mkuu.