MWENYEKITI wa Jumuiya ya Vijana wa Chama Cha Mapinduzi CCM (UVCCM) Mkoa wa Kagera Faris Buruhani amesema katika pindi cha miaka minne ya Rais Samia Suluhu Hassan serikali imefanikiwa kupandisha bei ya kahawa kutoka Sh. 1,200 hadi Sh. 5,000 na kuongeza thamani ya zao hilo.
Faris amebainisha hayo leo, Machi 13, 2025 wakati akizungumza na wananchi wa Kata ya Kibingo, wilayani Kyerwa, mkoani Kagera wakati wa ziara yake ya siku 16 katika wilaya zote za mkoa huo.
"Tuache sasa tabia ya kuwachagua viongozi wa vyama vya upinzani bali CCM ambacho kimeleta mageuzi makubwa katika zao kubwa la mkoa wetu," amesema Faris.
Katika hatua nyingine Faris amekemea usaliti katika chama hicho unaofanywa pindi unapokaribia uchaguzi mkuu bali wawe na mapenzi mema kwa wagombea hicho.
© 2025 IPPMEDIA.COM. ALL RIGHTS RESERVED