Kiongozi wa Chama cha ACT Wazalendo, Dorothy Semu, na Mwenyekiti wa Taifa wa Chama, Othman Masoud Othman, wamesafiri kuelekea Angola, ambako watashiriki mazungumzo ya Jukwaa la Demokrasia Afrika (The Platform for African Democrats - PAD), leo tarehe 13 Machi 2025.
Mbali na viongozi hao wakuu, ujumbe wa ACT Wazalendo pia unawajumuisha:
✅ Dk. Nasra Omar – Naibu Katibu wa Idara ya Mambo ya Nje na Waziri Kivuli wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa.
✅ Ndg. Pavu Abdalla Juma – Katibu wa Idara ya Haki za Binadamu na Vyombo vya Uwakilishi, ambaye pia ni Waziri Kivuli wa Utawala Bora na Muungano.
Mazungumzo hayo yameandaliwa na The Brenthurst Foundation, yakilenga kuwaleta pamoja wanademokrasia wa Afrika kwa ajili ya kutafakari masuala ya demokrasia, kubadilishana uzoefu, na kuimarisha mikakati ya kukuza demokrasia barani Afrika.
Mkutano huo utahudhuriwa pia na viongozi mashuhuri wakiwemo:
✅ Ian Khama – Rais wa zamani wa Botswana.
✅ Andrés Arango – Rais wa zamani wa Colombia.
✅ John Steenhausen – Waziri wa Kilimo wa Afrika Kusini na Kiongozi wa Chama cha DA cha Afrika Kusini.
✅ Venancio Mondlane – Kiongozi wa Chama cha PODEMOS, Msumbiji.
Mkutano huo unatarajiwa kufikia hitimisho kwa kupitishwa kwa mpango wa utekelezaji kuhusu hali ya demokrasia barani Afrika.
© 2025 IPPMEDIA.COM. ALL RIGHTS RESERVED