Bodi ya TANESCO yamlilia Mhandisi Nyamo-Hanga

By Mwandishi Wetu , Nipashe Jumapili
Published at 02:42 PM Apr 13 2025
Mhandisi Gissima Nyamo-Hanga.
Picha: Mtandao
Mhandisi Gissima Nyamo-Hanga.

Bodi ya Wakurugenzi wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) imethibitisha taarifa za kifo cha Mkurugenzi Mtendaji wa shirika hilo, Mhandisi Gissima Nyamo-Hanga, kilichotokea leo Jumapili, Aprili 13, 2025, kufuatia ajali ya gari katika Wilaya ya Bunda, mkoani Mara.

Kupitia taarifa rasmi iliyotolewa na TANESCO, shirika hilo limeeleza masikitiko makubwa na kutoa pole kwa familia ya marehemu, ndugu, jamaa, wafanyakazi wote wa TANESCO pamoja na Watanzania kwa ujumla, likieleza kuwa kifo cha Mhandisi Nyamo-Hanga ni pigo kubwa kwa taifa.

“TANESCO inasikitika kutangaza msiba huu mzito na kuungana na Watanzania wote katika kipindi hiki cha maombolezo,” imesema sehemu ya taarifa hiyo.

Aidha, shirika hilo limeeleza kuwa taarifa zaidi kuhusu ratiba ya shughuli za maombolezo pamoja na taratibu za mazishi zitatolewa kadri mipango itakavyokamilika.

Taarifa.