Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), John Heche amesema chama hicho kitaendeleza kampeni ya no reforms no election yaani bila mabadiliko hakuna uchaguzi ila kuhakikisha kwamba mabadiliko hayo yanapatikana.
Akizungumza na wanachama wa chama hicho mkoani Mbeya jana, Heche amesema hawatakata tamaa licha ya Mwenyekiti was kutiwa nguvuni na hivyo kushindwa kuendelea na kampeni hiyo.
“Nataka niseme mbele yenu mimi ambaye nimebaki nasimamia chama hiki sitarudi nyuma tunasonga mbele, hatutabaki kuomboleza Lissu kukamatwa, atakaa ndani sisi wengine tutasonga mbele”-alisema Heche
© 2025 IPPMEDIA.COM. ALL RIGHTS RESERVED