Mgombea Mwenza wa Urais CCM, Balozi Dk. Emmanuel Nchimbi amesema kura kwa mgombea urais, wabunge na madiwani wa CCM ni kura ya kuimarisha umoja na kuhakikisha kila kijiji na kata inafikiwa na huduma bora.
Amesema hayo katika mkutano wa kampeni za Uchaguzi Mkuu uliofanyika katika Uwanja wa Polisi Himo, ambapo pamoja na mambo mengineyo aliwanadi na kuwatambulisha wagombea wa CCM katika eneo hilo.
Akiwaombea kura wagombea hao, Dk. Nchimbi anasema wagombea hao wanawakilisha dira ya CCM ya kuwaletea wananchi maendeleo kupitia utekelezaji wa iIani ya Uchaguzi ya mwaka 2025-2030
Akizungumza kwa niaba ya wagombea wenzake, mbunge mteule wa Jimbo la Vunjo, Enock Koola anasema changamoto kubwa zinazowakabili wananchi wa jimbo hilo ni barabara na upatikanaji wa maji safi.
Anasema wananchi wanachokitaka miaka mitano ijayo ikiwemo kushirikiana na Serikali kuhakikisha barabara za Chekereni–Kahe–Mabogini, Pofo–Mandaka–Kilema na Uchira–Kisomachi zinajengwa kwa kiwango cha lami pamoja na kukamilisha miradi ya maji inayosuasua.
© 2025 IPPMEDIA.COM. ALL RIGHTS RESERVED