MGOMBEA Urais wa Zanzibar kwa tiketi ya CCM Dk Hussein Ali Mwinyi amesema kuwa historia inaonesha kuwa katika chaguzi zilizopita ndoa huvunjika na wanandoa hutwangana talaka kwa kisingizio cha uchaguzi.
Amesema uchaguzi isiwe chanzo cha mifarakano katika ndoa na katika nchi hivyo ni vyema wananchi kuwa wamoja na kudumisha amani ya nchi. Ameyasema hayo leo Septemba 14 wakati akizungumza na viongozi wa dini wa madhehebu mbalimbali na wazee wastaafu katika mkutano wake wa kunadi sera uliofanyika katika ukumbi wa Shekhe Idrisa Abdulwakil Mjini Zanzibar.
Amesema miaka iliyopita kipindi kama hiki cha kampeni Zanzibar huwa na machafuko na mifarakano ya kisiasa na kuwa na matabada kutokana na itikadi za kisasa lakini katika kampeni za mwaka huu hadi sasa hali ni shwari hivyo ni vyema kuendeleza umoja na mshikamano huo.
Mgombea huyo ambae pia ni Rais wa Zanzibar, amewataka wananchi kuendelea kumuunga mkono na kumchagua katika uchaguzi mkuu ili kuwatumikia tena kwa kipindi cha pili.
© 2025 IPPMEDIA.COM. ALL RIGHTS RESERVED