Miradi ya maendeleo yenye thamani ya Sh. bilioni 18.5 kuzinduliwa Morogoro

By Christina Haule , Nipashe Jumapili
Published at 11:14 AM Apr 13 2025
MKUU wa Mkoa wa Morogoro, Adam  Malima amesema Mwenge wa Uhuru Kitaifa  unatarajiwa kupitia na kuzindua miradi 70 iliyopo katika halmashauri 9 za mkoa wa Morogoro yenye jumla ya thamani ya Shilingi Bilioni 18.5
PICHA: CHRISTINA HAULE
MKUU wa Mkoa wa Morogoro, Adam Malima amesema Mwenge wa Uhuru Kitaifa unatarajiwa kupitia na kuzindua miradi 70 iliyopo katika halmashauri 9 za mkoa wa Morogoro yenye jumla ya thamani ya Shilingi Bilioni 18.5

MKUU wa mkoa wa Morogoro Adam Malima amesema Mwenge wa Uhuru Kitaifa unatarajiwa kupitia na kuzindua miradi 70 iliyopo katika halmashauri 9 za mkoa wa Morogoro yenye jumla ya thamani ya Shilingi Bilioni 18.5

Malima amesema hayo wakati akipokea Mwenge huo kutoka mkoani Pwani ambapo amesema mkoa unaendelea na kampeni za kupambana na madawa ya kulevya, kupunguza maambukizi mapya ya UKIMWI na Malaria.

Ukiwa wilayani Morogoro Mwenge wa Uhuru umezindua mradi wa maji wenye thamani ya shilingi milioni 334 uliojengwa na Wakala wa usambazaji maji na usafi wa mazingira Vijijini (RUWASA) katika kijiji cha Diguzi kilichopo wilayani Morogoro.

Akizindua mradi huo kwa kuweka jiwe la msingi kiongozi wa mbio za Mwenge wa Uhuru kitaifa Ismail Ussi leo amesema mradi huo utaenda kunufaisha wakazi zaidi ya 2,453 katika kijiji hicho.

Aidha baadhi ya wakazi wa kijiji hicho akiwemo Baraka Mbogera wamemshukuru na kupongeza juhudi za Raisj Dk. Samia Suluhu Hassam kwa kuwaondolea changamoto ya maji ambayo ilikuwa ikiwasumbua kwa muda mrefu.