Kipyenga cha kuwania Urais wa Zanzibar katika Uchaguzi Mkuu Oktoba 2025 wa Chama cha ACT-Wazalendo kimeshapulizwa ambapo Mwenyekiti wa Chama hicho, Othman Masoud Othaman amechukua fomu ya kuwania nafasi hiyo.
Othman ambaye pia ni Makamu wa Kwanza wa Rais leo Arili 13,2025 majira ya saa 4.00 asubuhi amechukua fomu ya kugombea nafasi hiyo ikiwa ni mwanachama wa kwanza kwa nafasi ya urais kuchukua fomu hiyo.
Akiwa katika Ofisi kuu za chama hicho Vuga Mjini Zanzibar, Othman amekabidhiwa fomu hiyo na Katibu wa Kamati ya Uchaguzi ya ACT Wazalendo, Mhene Said Rashid.
Baada ya kukabidhiwa fomu hiyo, Othman amesema amefaya uwamuzi huo ni sehemu muhimu katika chama na uchaguzi ni mchakato na kabla ya kuingia katika bahari kubwa ya kitaifa huwa kuna mchakato katika chama.
Amesema chama kinachombo kinachosimamia mchakato huo na maandalizi ni mazuri katika kusimamia mchakato wa uchukuaji wa fomu kwa nafasi mbalimbali.
"Leo sio siku ya kuzungumza ,nitakuja kuzungumza siku ambayo nitarejesha fomu April 16 mwaka huu"alisema Othman.
Chama hicho ni miongoni mwa nyama 18 vilivyosaini kanuni za maadili ya uchaguzi 2024 ambazo zitatumika kwenye uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani.
© 2025 IPPMEDIA.COM. ALL RIGHTS RESERVED