Waziri wa Viwanda na Biashara, Dk. Seleman Jafo, amesema Tanzania kwa sasa ina jumla ya viwanda 13 vya kuunganisha magari, ikiwa ni hatua muhimu ya kuimarisha sekta ya viwanda nchini kupitia uzalishaji wa ndani.
Dk. Jafo alitoa kauli hiyo leo wakati akiwasilisha hotuba ya makadirio ya mapato na matumizi ya Wizara ya Viwanda na Biashara kwa mwaka wa fedha 2025/2026 Bungeni jijini Dodoma.
Ameeleza kuwa kati ya viwanda hivyo, viwili (2) vinaunganisha magari kamili, ambavyo ni:
Waziri Jafo ameongeza kuwa viwanda 11 vilivyosalia vinafanya kazi ya kutengeneza matrela, vinavyosaidia pia kukuza ajira na kuongeza thamani ya bidhaa zinazotumika katika sekta ya usafirishaji.
Aidha, Waziri ameeleza kuwa ujenzi wa kiwanda cha TATA unaendelea katika eneo la TAMCO, Kibaha mkoani Pwani. Hadi kufikia Machi 2025, ujenzi huo ulikuwa umefikia asilimia 70. Kiwanda hicho kinatarajiwa kuunganisha vichwa vya magari, magari ya mizigo aina ya tipa, pamoja na pikipiki. Uwekezaji wake unakadiriwa kufikia Shilingi bilioni 19.
Waziri Jafo amesisitiza kuwa Serikali itaendelea kuweka mazingira wezeshi kwa wawekezaji katika sekta ya magari na viwanda kwa ujumla, ili kuongeza ajira, kupunguza utegemezi wa bidhaa kutoka nje na kuchochea maendeleo ya viwanda nchini
© 2025 IPPMEDIA.COM. ALL RIGHTS RESERVED