Zaidi ya magari 200 yamekwama katika eneo la Chamakweza, Halmashauri ya Chalinze, mkoani Pwani, kufuatia ajali ya lori lililoanguka na kuziba barabara.
Tukio hilo limetokea leo asubuhi na kusababisha msongamano mkubwa wa magari kwenye Barabara Kuu ya Dar es Salaam–Morogoro, hali iliyosababisha usumbufu mkubwa kwa wasafiri na wafanyabiashara wanaotumia njia hiyo muhimu ya kiuchumi.
Kwa sasa, Jeshi la Polisi kupitia Kitengo cha Usalama Barabarani linaendelea na jitihada za kuondoa lori hilo lililopata ajali, ili kuruhusu magari mengine kuendelea na safari.
© 2025 IPPMEDIA.COM. ALL RIGHTS RESERVED