KATIBU wa NEC, Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa CCM Taifa, CPA Amos Makalla, amesema wamewakubalia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kupumzika.
Aliyasema hayo leo wakati akizungumza na wananchi wa Tarafa Lionja, Kata Lionja, Wilaya ya Nachingwea, mkoani Lindi, waliofika kumpokea kwa ajili ya mwendelezo wa ziada yake ya siku 10 katika mikoa ya Lindi na Mtwara.
“Na uzuri niseme nisiseme, wanapumzika wamechoka huu mwendo hawauwezi na sisi tumewakubalia," amesema.
Makalla amewapa pole wananchi kwa matusi na kejeli na kuwaeleza wamekuja wao wenye dhamana nao kuwaelezea miradi iliyotekelezwa na serikali.
Kadhalika amewaeleza namna nchi inavyoelekea kwenye maendeleo, huku akiwasisitizia kwamba, amani na utulivu imeasisiwa na Chama Cha Mapinduzi.
© 2025 IPPMEDIA.COM. ALL RIGHTS RESERVED