Kanuni za maadili kisiwe kigezo cha kuzuia chama kushiriki uchaguzi-Ado Shaibu

By Enock Charles , Nipashe
Published at 01:56 PM Apr 12 2025
Katibu Mkuu wa Chama cha ACT-Wazalendo, Ado Shaibu
PICHA: MTANDAO
Katibu Mkuu wa Chama cha ACT-Wazalendo, Ado Shaibu

Katibu Mkuu wa Chama cha ACT-Wazalendo, Ado Shaibu amependekeza kwamba chama ambacho hakitasaini kanuni za maadili ya uchaguzi kisizuiwe kushiriki uchaguzi huo kwa kuwa ni haki ya Kikatiba.

Akieleza mapendekezo ya chama hicho ambayo chama hicho kimeyawasilisha katika Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi katika hafla ya utiaji saini kanuni za maadili jijini Dodoma leo, Ado ameitaka tume kumpa ufafanuzi wa mapendekezo ya chama hicho kabla ya kutia saini kanuni hizo.

“ACT-Wazalendo tuliwasilisha mani kwamba haki ya chama cha siasa kushiriki uchaguzi ni ya kikatiba, kusaini (kanuni za maadili) kuwe ni ‘commitment’ tu peke yake na siyo kukiondolea chama haki ya kushiriki katika uchaguzi” amesema Ado