KATIBU Mkuu wa Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM) Taifa, Jokate Mwegelo, amewataka wanawake mkoa wa Shinyanga kushiriki na kugombea nafasi mbalimbali za uongozi katika uchaguzi mkuu mwaka huu, ili kupata viongozi wa kuwasema chagangamoto zao.
Pia, amewataka kumuunga mkono Rais Samia Suluhu Hassan katika kumpigia kura, ili kuendelea kupata ridhaa ya kuongoza kwa awamu nyingine, kwa kuwa alipokea nchi katika wakati mgumu, watu wachache walimbeza na sasa anafanya makubwa kuliko walivyotarajia.
Rai hiyo ametoa wakati wa Tamasha la Tuzo la Mwanamke Chuma 2025, zilizoandaliwa na kutolewa na kituo cha Radio cha Gold Fm cha mjini Kahama na kusisitiza kila mmoja mwenye sifa anawajibu wa kushiriki uchaguzi na kugombea, ili kupata viongozi.
Aidha Jokate, amewashauri kuchangamkia fursa za mikopo inayotolewa halmashauri kupitia asilimia 10 ya mapato ya ndani katika kujiinua kiuchumi na kuondokana na utegemezi kwenye familia, kwani usawa la asilimia 50/50 unataka kila mmoja kutafuta kipato na sio kutegemeana.
Mkuu wa Wilaya ya Kahama, Mboni Mhita, aliunga mkono hoja hiyo na kusema, halmashauri za Msalala, Ushetu na Manispaa ya Kahama, zimetenga zaidi ya Sh. bilioni mbili, kwa ajili ya kutoa mikopo isiyokuwa na riba kwa kundi la wanawake, vijana na watu wenye ulemavu.
"Kahama ni mji wa kibiashara na una fursa nyingi ambazo wanawake zinaweza kutunufaisha, tutumieni tamasha hili kupeana mawazo, fursa, ujuzi na uzoefu katika biashara tunazozifanya. Tumeona wengi wetu wamefika mpaka katika sekta ya madini ambapo awali haikuwa rahisi kuwaona,” amesema Mhita.
Mwaandaji wa Tamasha la Mwanamke Chuma 2025, Neema Mghen, amesema mpaka sasa wameweza kuwafikia wanawake zaidi ya 100,000 katika mkoa wa Shinyanga na kuwaunganisha na fursa mbalimbali za kiuchumi ambazo zimeanza kuleta matokeo chanya,
© 2025 IPPMEDIA.COM. ALL RIGHTS RESERVED