WANANCHI wa Kijiji na Kata ya Mangae Tarafa ya Mlali, wilayani Mvomero, wameanza kunufaika na mradi wa maji uliojengwa na Wakala wa Usambazaji Maji Vijijini (RUWASA), wenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 600, ambao umezinduliwa na mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa 2025.
Mmoja wa wananchi wa kijiji hico, Emiliana Costantine, anasema wamekuwa wakisumbuka kupata huduma ya maji hata yasiyo salama na kulazimika kutembea umbali mrefu, kufuata ya visima kutokana na jiografia ya eneo lao lilivyo.
Hivyo anaishukuru serikali kwa kuwasaidia kupata maji, wameanza kusambaziwa mabomba kwenye maeneo yao na kwamba yanawasaidia kutumia muda waliotumia kutafuta maji kufanya shughuli nyingine za maendeleo.
Mkuu wa Wilaya ya Mvomero, Judith Nguli, amesema jumla ya miradi saba yenye thamani ya shilingi bilioni 1.8 inatarajiwa kutembelewa na kuzinduliwa na Mwenge wa Uhuru, unaokimbizwa mkoani Morogoro kwa sasa.
Mkoa wa Morogoro ni mkoa wa pili katika kuupokea na kuukimbiza Mwenge wa Uhuru mwaka 2025, ulioasisiwa na Rais wa awamu ya kwanza Baba wa Taifa Hayati Mwalimu Julius Nyerere, mwaka 1961.
© 2025 IPPMEDIA.COM. ALL RIGHTS RESERVED